Magoli ya Simba SC yamefungwa na Leonel Ateba Mbida aliyefunga dakika ya 35 na 45 kipindi cha kwanza magoli hayo Ateba amefikisha magoli 5 katika ligi kuu Tanzania bara akionekana kuendelea kuimarika kadri siku zinavyozidi kwenda akiwa na kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.
Timu ya Wekundu wa Msimbazi imepata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya kikosi cha KenGold kutoka mkaoni Mbeya mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex Mwenge Dar es salaam.
Magoli ya Simba SC yamefungwa na Leonel Ateba Mbida aliyefunga dakika ya 35 na 45 kipindi cha kwanza magoli hayo Ateba amefikisha magoli 5 katika ligi kuu Tanzania bara akionekana kuendelea kuimarika kadri siku zinavyozidi kwenda akiwa na kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.
Ushindi huo umekifanya kikosi hiko kinachonolewa na Kocha Fadlu Davies kufikisha alama 31 kikiwa nafasi ya pili alama mbili nyuma ya timu ya Azam FC inayoongoza ligi ikiwa na alama 33 ikiwa imecheza michezo mitatu zaidi ya Simba SC.
Fadlu Davies ameendelea na utaratibu wake wa kufanya mzunguko kwa Wachezaji wake baada ya kupumzisha baadhi ya nyota Wake walioanza kwenye mchezo uliopita wa hatua ya makundi dhidi ya kikosi cha CS Sfaxien siku ya Jumapili.
Mzamiru Yasin alianza kwenye kikosi cha kwanza baada ya kukosekana kwa muda mrefu Mohamed Hussein Zimbwe Junior na Shomari Kapombe nao wameanzia nje kwenye mchezo wa leo.
Wapinzani wao wa jadi kikosi cha Yanga SC chenyewe kitashuka dimbani kesho kucheza dhidi ya Mashujaa FC kutokea mkaoni Kigoma mchezo utachezwa uwanja wa KMC Complex Mwenge Dar es salaam.