Mfungaji bora huyo wa mashindano ya kombe la Dunia la mwaka 2002 atashindana na Rais wa sasa wa CBF Ednaldo Rodrigues katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 2026.
Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Ronaldo Nazario Di Lima ametangaza kuwania Urais wa shirikisho la mpira nchini Brazil Brazilian Football Confederation ( CBE ).
El Phenomenon kama alivyokuwa akifahamika kipindi anacheza soka alipewa jina hilo kutokana na umahiri wake wa kusakata kabumbu akiwa na timu ya taifa ya Brazil The Samba Boys na vilabu vya Inter Milan ya Italia, Real Madrid na Barcelona vyote vya Hispania PSV ya Uholanzi na Cruzeiro ya nchini Brazil.
Ronaldo ametangaza niya yake ya kugombea nafasi hiyo ya Urais mapema leo siku ya Jumanne tarehe 17 Disemba akiwa nchini kwao Brazil.
Sababu kubwa iliyomfanya mshindi huyo wa kombe la Dunia mara mbili 1994 na 2002 ni kutaka kuirudisha heshima ya Brazil ambayo imepotea kwa siku za karibuni.
Mfungaji bora huyo wa mashindano ya kombe la Dunia la mwaka 2002 atashindana na Rais wa sasa wa CBF Ednaldo Rodrigues katika uchaguzi mkuu utakaofanyika 2026.
Ronaldo ametangaza kuuza timu yake anayoimiliki ambapo kwasasa yupo kwenye hatua ya mwisho ya mazungumzo kuuza timu ya Real Valladolid ili kuondoa pingamizi la yeye kutimiza azima yake kuliongoza shirikisho la mpira nchini Brazil CBF.
Timu hiyo bingwa mara tano wa kombe la Dunia haijashinda kombe hilo tangu mara ya mwisho ifanye hivyo mwaka 2002 katika fainali zilizofanyika kwa uuandaji wa pamoja wa nchi za Korea kusini na Japan.
Kikwazo kikubwa kinachotajwa kuifanya Brazil kushindwa kutwaa taji hilo kwa muda mrefu ni sera mbaya ya shirikisho la mpira la nchi hiyo kushindwa kuandaa mipango ya kuzalisha Wachezaji wenye uwezo mkubwa kuliko Wapinzani wao.
Lakini pia kuondoka kwenye utamaduni wa soka lao na kufata tamaduni za soka la nje ya Brazil zinaifanya timu hiyo kuhangaika kushinda ubingwa wa Dunia Ronaldo amedhamiria kutaka kurudisha heshima ya Brazil kama taifa lililokuwa likiogopwa na Wapinzani kutokana na ubora wa Wachezaji wake.
Je Ronaldo atakuwa Muarobaini wa changamoto za soka nchini Brazil ataweza kutatua changamoto hizo na kuifanya timu hiyo kushinda tena kombe la Dunia muda unaweza ukawa na majibu sahihi tusubiri atakapoingia madarakani 2026.