Klabu ya Manchester United ya Uingereza imetangaza kumfuta kazi kocha wake Erik Ten Hag. Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Ten Hag amepata taarifa ya kufutwa kwake kazi asubuhi ya leo baada ya jana kupoteza mchezo wa ligi kuu Uingereza ugenini uwanja wa London Stadium nyumbani kwa timu ya West Ham United.
Klabu ya Manchester United ya Uingereza imetangaza kumfuta kazi kocha wake Erik Ten Hag. Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Ten Hag amepata taarifa ya kufutwa kwake kazi asubuhi ya leo baada ya jana kupoteza mchezo wa ligi kuu Uingereza ugenini uwanja wa London Stadium nyumbani kwa timu ya Westham United.
Kocha huyo raia wa Uholanzi alijiunga na Man United mwaka 2021 akitokea timu ya Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi. Amekiongoza kikosi cha Mashetani Wekundu kushinda ubingwa wa FA msimu uliopita 2023-2024 na kombe la ligi ( EFL) 2022-2023.
Kikosi cha United kimepata matokeo ya ushindi kwenye mchezo mmoja kati ya michezo nane iliyocheza kwenye mashindano yote. Kipigo dhidi ya Wagonga Nyundo wa jiji la London kimepelekea Mabosi wa klabu hiyo Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Uingereza kufanya maamuzi ya kumfuta kazi Mholanzi huyo.
Ten Hag alipewa michezo miwili kuokoa kibarua chake kabla ya ligi kusimama kupisha michezo ya kimataifa kwa timu za taifa, alifanikiwa kushawishi Viongozi wa United kumvumilia kutokana na kutopoteza michezo hiyo ya FC Porto na Aston Villa.
Manchester United inashika mafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza ikiwa imeshinda michezo mitatu, imetoka sare michezo mitatu na kupoteza michezo minne.Kikosi hiko kitakuwa chini ya Kocha wa muda raia wa Uholanzi ambaye alishawahi kucheza kwenye timu hiyo nafasi ya ushambuliaji Ruud van Nistelrooy.
Michezo mitano ijayo ya United kwenye mashindano yote Oktoba 30, dhidi ya Leicester City mchezo wa kombe la ligi, Novemba 3, dhidi ya Chelsea mchezo wa ligi kuu Uingereza, Novemba 7 dhidi ya PAOK mchezo wa Europa, Jumapili Novemba 10 itacheza uwanja wa Old Trafford ikiwakaribisha Leicester City kwenye muendelezo wa ligi kuu ya Uingereza.