Alhamisi , 19th Sep , 2024

Meneja Habari na Mawasiliano Simba  SC Ahmedy Ally amesema kuwa ameona   wapinzani wao Al Ahly Tripoli  wameshaingia  Dar es salaam tena wamekuja na mabaunsa na hivyo wamedharia ubaya ubwela katika mchezo huo wa mkondo wa pili wa kombe la shirikisho utaopigwa jumapili hii

“Wapinzani wetu (Al Ahly Tripoli) wameshaingia nchini na mkwala mzito, wamekodi mabaunsa wengi kwelikweli kwa kutambua ugumu ulipo. Sisi ni wengi kuliko mabaunsa wao, tunapaswa kwenda kuwaonyesha kwamba pamoja na wote mliokodi hamuwezi kufanya lolote mbele ya Nguvu Moja ya Simba Sports Club.”  Ahmed Ally,  Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC

Septemba 22 2024 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa wakiwa na kumbukumbu ya kutoshana nguvu kwenye mchezo uliopita wakiwa ugenini kwa ubao kusoma 0-0