Jumamosi , 27th Jul , 2024

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mvomero Bw. @saidnguya akiwa katika Shule ya Sekondari Lusanga na Diongoya, Nguya amewataka wanafunzi kutokubali kuchakachuliwa, kwani kukubali hilo kutawafanya kutoyatimiza malengo yao waliojiwekea.

"Watu wote waliofanikiwa kufikia malengo yao, kuwa wafanyabiashara mashuhuri, kuwa viongozi imara, kuwa wanasayansi wabobevu, hawakukubali kuchakachuliwa kwa huu kama wa kwenu, walijichunga na sasa wamefikia kwenye matarajio yao" amesisitiza Nguya.

Katika hatua nyingine, Afisa kutoka Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Yahaya Tumba amewasiistiza wanafunzi kuwa na maadili mema, kwani ndoto zao walizo nazo, msingi wake ni maadili yalio mema, hivyo ni vema wakawa wasikivu wa walimu wao, wazazi na walezi Ili kuyafikia malengo yao.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mvomero Bw. @saidnguya akiwa ameambatana na viongozi wa dini, maafisa Halmashauri na kutoka Tume ya Taifa ya Maadili kwa Umma na wadau wengine wametembelea shule za Diongoya na Lusanga Sekondari, Lusanga na Muungano Shule za Msingi katika muendelezo wa Kampeni ya kutoa elimu kwa wanafunzi kujiepusha na kujikinga dhidi ya vitendo vya ukatili na mmomonyoko wa maadili.