Japhet Koome
Hatua hii inajiri kufuatia mauaji ya vijana wanaojiita 'Gen Z' yaliyofanywa na polisi wakati wa maandamano ya kupinga muswada wa fedha pamoja na yale ya kupinga serikali iliyopo madarakani yaliyoenda kwa takribani majuma matatu.
Mara baada ya baadhi ya vijana waandamanaji nchini humo kuuawa kwa kufyatuliwa risasi na polisi huku wengine wakiachwa na majeraha ya risasi, wananchi pamoja na viongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja nchini Kenya walitoa rai kwa IGP huyo kujiuzulu kwa kile walichokidai kuwa ameruhusu Askari wake kufanya mauaji kwa vijana walioamua kuandamana kwa amani.