Jumapili , 16th Mar , 2014

Nazizi ambaye hivi sasa ameamua kulea mtoto wake kivyake baada ya kutalakiana na aliyewahi kuwa mume wake Vini, amekerwa na habari zilizotapakaa kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na mgao wa mali walizochuma pamoja ndani ya ndoa.

Nazizi ameongea hayo kupitia mahojiano yaliyofanyika nchini humo akisema kuwa yeye na Vini wameishi miaka mitano ya ndoa yao na hakuwahi kuwaza kuwa mali ndilo jambo ambalo limemfanya Nazizi kutalikiana na mumewe bali ni maamuzi ambayo wao kwa pamoja wameyaafiki na kuamua na familia za pande zote mbili.

Hivi sasa Nazizi amesema kuwa yupo mbioni kuzindua wimbo wake mpya ndani ya albamu yake iliyobatizwa jina ‘Nazizi Evolussion’ wimbo ambao utakuwa ni singo itakayotoka ndani ya wiki mbili zijazo.