Jumatatu , 26th Feb , 2024

Mwanumuziki Peter Morgan (Peetah) ambaye alikuwa mwimbaji kiongozi kwenye kundi la muziki wa Reeage la Morgan Heritage nchini Jamaica amefariki dunia usiku wa jana Jumapili. Familia ya mwanamuzki huyo imethibitisha taarifa hizo japo hawajaweka sababu za kifo chake.

-
Akiwa na ndugu zake katika kundi la Morgan Heritage, Peter aliwahi kushinda tuzo ya Grammy kupitia albamu yao ya Strictly Roots katika kipengele cha Albamu Bora ya Reggae mwaka 2016.
-
Itakumbukwa pia Peetah kupitia kundi la Morgan Heritage aliwahi kufanya kazi na wasanii kama Diamond Platnumz na Harmonize wa hapa Tanzania.