Alhamisi , 25th Jan , 2024

Muigizaji na rapa 50 Cent amenyoosha maelezo kuhusu picha hiyo ambayo amepost siku 3 zilizopita baada ya mashabiki zake kudai staa huyo amepungua kilo kadhaa kwenye mwili wake.

Picha mpya ya 50 Cent baada ya kupungua kilo 18

Comments hizo zimemfikia 50 Cent amejibu hilo kwa kukiri kwamba kupungua kutoka Pound 250 (kilo 113) mpaka Pound 210 sawa na kilo 95.

50 Cent amesema chanzo cha kupungua kilo hizo ni kupiga sana GYM pamoja na ziara yake ya kimuziki ‘The Final Lap Tour’ ambayo alizunguka nchi kadhaa.