Jumanne , 9th Jan , 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, ameitaka Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) kuja na ubunifu wa kujenga makazi bora ya watumishi wa umma katika maeneo ya mijini  jirani na maeneo ya shule na hospitali

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene

ili kuwaondolea changamoto ya makazi manesi na walimu  kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao.

Amesema maeneo ya mijini, shule pamoja na hospitali zinamiliki maeneo makubwa ambayo taasisi ya WHI inaweza kuyatumia kujenga majengo marefu kwenda juu ili kuwafanya walimu na  manesi wafurahie kutoa huduma kwa wananchi kwa kuishi kwenye makazi bora jirani na maeneo ya kazi 

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Timu ya Menejimenti ya Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) ikiwa ni muendelezo wa kusikiliza changamoto zinazoikabili Taasisi anazozisimamia  pamoja na kufuatilia  utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara aliyoifanya Mwezi Agosti mwaka jana

"Hakuna asiyejua umuhimu wa walimu na manesi katika nchi hii lakini lakini wengi wao wamekuwa wakiishi maeneo ya mbali na wanakofanyia kazi na hivyo kulazimika kulipa nauli kubwa kwa vile hawawezi kumudu kulipa kodi ya makazi yaliyo jirani na maeneo yao ya kazi, waguseni hawa kwa kuwajengea makazi bora," amesema Waziri Simbachawene