
Mafuriko
Eneo kubwa lililoathiriwa na hayo ni kata ya Gendabi ambapo nyumba za watu zimezingirwa na maji na miti iliyosombwa na mafuriko yaliyopelekea barabara ya Bababti kwenda Singida katika eneo la Kates kushindwa kupitika kwa muda.
Shughuli za uokozi zinaendelea zikiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga na kamati ya ulinzi na usalama.