
Google kwa sasa wamepanga kuja na programu maalumu ambayo itamuwezesha mtumiaji wa mitandao kuweza kubaini
a) Kama picha hiyo ni yenye uhalisia (si ya kutengeneza)
b) Historia ya picha hiyo ikijumuisha siku iliyotengenezwa.
c) Wavuti ambazo zimetumia picha hizo/hiyo
d) watu wengine wametoa taarifa gani kuhusiana na picha hiyo/hizo
Baadhi ya wavuti ambazo zimekuwa zikitumika kwenye utengenezaji wa picha zisizo na uhalisia ni pamoja na Firefly, Midjourney,Nightcafe,Dreamstudio na nyinginezo.
Picha: BDM chanzo: techcrunch