Ijumaa , 13th Oct , 2023

Shirikisho la Ngumi Duniani (WBA) limetupilia mbali maombi ya Bondia Muingereza Daniel Dubois kupitia kwa promota wake Frank Warren ya kutengua ushindi alioupata dhidi ya bondia Oleksandr Usyk kwenye mchezo uliofanyika Agosti 26-2023 nchini Poland

Taarifa WBA imesema hakukuwa na ushahidi wa kutosha ili kubatilisha uamuzi wa awali huku kesi hiyo ilipelekwa kwenye kamati maalumu ya waamuzi na kujiridhisha kuwa Dubois alimdondosha Usyk kupitia ngumi iliyopigwa chini ya mkanda ambapo ni kinyume na sheria za ngumi duniani.

Oleksandr Usyk anayeshikilia mikanda ya WBA,IBF na WBO alidondoshwa kwenye ulingo kwenye mzunguko 5 na kupewa dakika 4 za kukaa sawa kabla Dubois kuchapwa kwenye mzunguko wa 9 na kuitetea mikanda yake anayoishikilia kwa sasa.