Akizungumza na Wanahabari, Meneja Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmedy Ally amesema wanatambua utakuwa ni mchezo ni mgumu dhidi ya Power Dynamos, hivyo wanakuja Tanzania, sehemu ambayo hakuna aliyetoka salama.
“Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wpao wengine hawaujui."- Ahmed Ally. - Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC
Vile vile Ahmedy amesema Mechi yao dhidi Dyamos ya Zambia wataitumia kama maandalizi ya kuuendea mchezo wa Ufunguzi wa mashindano African Football League dhidi ya Al Ahly yanayotaraji kuanza kutimua vumbi Oktoba 20, 2023 katika uwanja wa Benjamin MKapa, jijini Dar es salaam.
Simba SC inahitaji kupata ushindi wowote, suluhu ama sare ya bao 1-1 ili kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa mwaka 2023-24.