Jumatano , 25th Feb , 2015

Star wa muziki wa nchini Uganda, Pallaso hatimaye ameamua kuweka rekodi sawa kuhusu tetesi za mahusiano yake na msanii wa muziki Sheeba Karungi, na kusema kuwa ana mapenzi tele kwa mwanadada huyo lakini ni tofauti na wengi wanavyofikiri.

Pallaso na Sheeba

Pallaso amesema kuwa, hisia za upendo alizonazo kwa Sheeba zinatokana na namna ambavyo anamfahamu binafsi, akimmwagia masifa kuwa uzuri wake ni wa kushangaza.

Kauli hizi zinazidi kuwaacha mashabiki wa mastaa hawa katika sintofahamu hasa ikiwa inajulikana kuwa Pallaso ameoa na ni baba wa familia ya mtoto mmoja.