Jumatatu , 25th Sep , 2023

Nyota Muingereza Cameron Norrie ameondoshwa kwenye hatua ya eobo fainali ya michuano ya tenisi ya Zhuhai Open inayofanyika nchini China na Mrusi Aslan Karatsev kwa seti 2-0.

Norrie mwenye miaka 28 ambaye anakamata nafasi ya 17 kwa viwango vya ubora wa tenisi kwa upande wa Wanaume ameondoshwa kwa  7-6 (7-5) 7-6 (7-5) na Mrusi Aslan Karatsev anayeshikilia nafasi ya 63 kwa viwango vya ubora wa tenisi duniani

Mrusi Aslan Karatsev mwenye miaka  30 ambaye alimuondoa Muingereza Andy Murray katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo atacheza na Mjapan Yoshihito Nishioka kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano leo Septemba 25-2023.