Ijumaa , 15th Sep , 2023

Shaina Iddy(10) mkazi wa Majohe jijini Dar es Salaam, amewaomba Watanzania wamsaidie fedha za matibabu yake ya miguu ambayo hajawahi kutembea tangu azaliwe, hali ambayo inapelekea kukosa haki za msingi kama kusoma kwa sababu hana kifaa chochote kinachomuwezesha kutembea.

Shaina Iddy(10), mlemavu wa miguu

Mama wa mtoto huyo Fadhat Abdallah, amesema wamejaribu kwenda hospitali kumsaidia mtoto wao atembee lakini gharama ni kubwa familia imeshindwa kuipata hivyo ameomba kusaidiwa kiasi cha shilingi 1,210,000/=, kwa ajili ya viatu maalum vitakavyomsaidia kutembea.

Ukiguswa kumsaidia, tafadhali wasiliana na Mama wa mtoto kwa namba 0789 912 627 jina ni HAWA HASSAN