Jumatatu , 4th Sep , 2023

Rais Emmerson Mnangagwa amekula kiapo cha urais, mwanzoni mwa muhula wake wa pili, akiapa kusimamia katiba.

Aliapishwa na Jaji Mkuu Luke Malaba mbele ya maelfu ya wafuasi kutoka chama chake cha Zanu-PF.

Viongozi wa kikanda akiwemo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na kiongozi wa Msumbiji Filipe Nyusi wanahudhuria hafla hiyo, vivyo hivyo pia ni mke wa rais wa zamani Grace Mugabe.

Chama chake cha Zanu-PF kilishinda karibu theluthi mbili ya kura za bunge.

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe kimethibitisha kuwa hakitataka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais mahakamani.

Matokeo rasmi yanaonyesha kuwa rais aliyeko madarakani Emmerson Mnangagwa alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita kwa karibu asilimia 53 ya kura, ambazo waangalizi wa kimataifa walisema zilipungukiwa na viwango vya kidemokrasia.