
Rais Samia Suluhu Hassan
Waziri Kairuki ametoa kauli hiyo leo wakati alikabidhi magari 10 ya Maafisa Elimu Sekondari yaliyonunuliwa kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).
"Wakati namuaga Rais kuwa leo nitakua Azania sekondari kwa ajili ya hafla ya ugawaji wa magari akaniambia anafahamu changamoto ya shule hii kuwa hakuna Patron kwa sababu hakuna nyumba ya shule anayoweza kuishi ili kuwa karibu na wanafunzi hao wakati wote hivyo ameelekeza nyumba hiyo ijengwe mara moja," amesema Waziri Kairuki