Ijumaa , 11th Aug , 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na (Sera, Bunge na Uratibu)  Jenista Mhagama, Ameitaka Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali, kuharakisha kutengeneza Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Utendaji wa Shughuli za Serikali

Pamoja na kukamilisha na kuzindua haraka Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini ndani ya nchi utakaotumika na Serikali kwa ujumla, Wizara, Taasisi na maeneo yote ya Utendaji kazi ndani ya Serikali.

Ameyasema hayo Jijini Arusha alipofungua Mkutano wa Mazingativu uliyohusisha, Viongozi, watumishi wa Ofisi hiyo Pamoja na Taasisi zake ambapo ameitaka pia idara hiyo kuwa na Ubunifu 
Aidha, Waziri Mhagama alisema anahitaji kupata taarifa ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Ofisi yake na Serikali kwa ujumla wa kila robo mwaka ikiwa ni katika kuboresha Eneo hilo.

Akizungumzia kuhusu Uchapishaji wa Nyaraka za Serikali, Waziri Mhagama amesema katika eneo hilo, katika mwaka huu Mpya wa Fedha 2023/2034, Serikali imejiwekea mkakati wa kuongeza Maduhuli na mapato yake kupitia Mpigachapa Mkuu wa Serikali, 

Akiongea katika Mkutano huo wa Mazingativu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt Jim Yonazi alisema kuwepo kwa Ofisi hiyo Jijini Arusha katika Mkutano huo  ni kutokana na nia ya Ofisi hiyo kuhakikisha kwamba inatenda majukumu yake kwa umakini na kwa utimilifu ikiwa ni pamoja na Uratibu wa shughuli za Serikali kwa ujumla na kwenye maeneo mengine.

Kwa Upande wake Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw. George Lugome alisema, kama Idara imejipanga hasa kwa watumishi kuhakikisha wanafanya kazi katika ubora wa hali ya juu na kuhakikisha, watumishi watapata mafunzo ya kuendesha mashine mpya za kisasa, kuongeza idadi ya watumishi wenye sifa na ueledi katika endeo hilo la uchapaji