Bangi zilizokamatwa
kuteketeza jumla ya hekari 489 ya mashamba ya bangi.
Katika wilaya ya Morogoro vijijini Kata ya Kisaki, Kijiji cha Rumba zimekamatwa gunia 70 za bangi, Kijiji cha Mbakana zimekamatwa gunia 59 na kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketezwa hekari 350 za mashamba ya bangi, aidha wilayani Mvomero mamlaka imeteketeza hekari 139 na wilaya ya Morogoro zimekamatwa gunia mbili (2) za bangi.
Akizungumza wakati wa operesheni hiyo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, wakulima wa bangi mkoani Morogoro wanalima pembezoni mwa mto, na kukata miti ili wawezekupata maeneo ya kulima bangi.
“Wakulima wa bangi wa mkoa huu wanachepusha maji na kuyazuia yasiende kwenye maeneo mengine yakahudumie wananchi ili kumwagilia mashamba yao, pia wanafanya uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti katikati ya msitu ili waweze kulima bangi, hivyo, wanafanya uharibifu mkubwa wa mazingira na kuharibu vyanzo vya maji katika maeneo haya," amesema Kamishna Jenerali Lyimo.