Jumatano , 2nd Aug , 2023

Zoezi la uokoaji wa miili ya watu waliokufa maji ndani ya Ziwa Victoria limekamilika hii leo Agosti 2, 2023, baada ya mwili wa mwisho kuopolewa na kufanya idadi ya waliopoteza maisha kufikia 14 ambapo miili yote itakabidhiwa kwa ndungu kwa ajili ya mazishi na serikali kusaidia kusafirisha.

Mwili ulioopolewa ziwani

Julai 30,2023 majira ya jioni mitumbwi miwili iliyokuwa imebeba waumini 28 wa Kanisa Takatifu la Mungu wa Kiroho (KTMK) ilizama ziwani ambapo watu 14 waliokolewa na kukimbizwa hospitalini.

Imeelezwa katika tukio hilo wengi walikuwa ni watoto na wanafunzi wa Shule ya Msingi Bulomba wilayani Bunda.