Ijumaa , 21st Jul , 2023

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Laalala kitongoji cha Kazingumu, wilayani Kiteto mkoani Manyara Amos Efael (38), ameuawa na wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kuiba mahindi shambani.

Mahindi

Amos alipoteza maisha akiwa Zahanati ya Matui wakati akipatiwa matibabu kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa wananchi

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Laalala Khalidi Soya Chubi, amesema awali mtuhumiwa huyo alikutwa na viroba vitatu vya mahindi ambayo hayajapukuchwa na kisha kupigwa na kundi la watu hao.

"Nilipata simu kutoka kwa mwananchi kuwa kuna mwananchi mmoja alionekana akiiba mahindi shambani na amezingirwa na watu, nikaenda huko ambapo niliwakuta na kuongozana naye mpaka kwa Mtendaji wa Kijiji na kuandikiwa barua kisha kwenda Zahanati ya Matui na huko alipofika akafariki," amesema Mwenyekiti