Ijumaa , 14th Mar , 2014

Kufuatia nyota ya msanii Lupita Nyong'o kuendelea kung'aa kimataifa kupitia fani ya uigizaji filamu, kiu ya kufahamu upande wa maisha yake binafsi imeendelea kuwa kubwa kwa mashabiki wa nyota huyo aliyetwaa tuzo maarufu ya oscar.

Taarifa juu ya staa huyu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki K'Naan zimeendelea kuchukua kasi siku hadi siku kwani wawili hao wamekuwa na ukaribu wa aina yake japokuwa inafahamika kuwa mwanamuziki huyu tayari ana watoto wawili na mke ambaye kwa sasa wametengana, na hivyo kutoa nafasi kubwa ya uwezekano wa kuanza kwa mahusiano mapya kwa mastaa hawa.

Lupita mwenyewe wala K'Naan bado hajathibitisha kama kuna ukweli katika taarifa hizi na mara ya mwisho Lupita kuulizwa kuhusu mahusiano, alisema kuwa kumekuwa na tetesi nyingi ambazo zina taarifa nyingi kiasi ambacho yeye binafsi anajiuliza kama zina ukweli ama la.