
Taarifa inasema kijana asubuhi ya Tarehe 07 Julai aliwasili ofisini kwake na kutoa taarifa kuwa hayupo vizuri kiafya.
Baada ya kurudi nyumbani alikimbia ghafla kutoka chumbani kwake akiwa mtupu huku damu nyingi zikimtoka katika eneo la uume wake na mbio hizo alizielekeza moja kwa moja katika eneo la bahari ambapo inadaiwa raia wema walimkuta akiwa anajiosha kidonda chake kwa maji ya bahari kwa dhumuni la kukata damu.
Aidha, inasemekana kijana Simoni alikutwa akiwa na pasi mkononi ambapo raia wema walimchukua na kwenda naye katika kituo cha Polisi ambapo katika mzunguko huo wote alionekana kimya pasi na kuzungumza neno lolote.
Rafiki zake wa karibu wanasema kijana huyo ni mgeni mjini Lindi, na inadaiwa ana matatizo ya akili ambapo hali hiyo humkuta mara nyingi awapo na msongo wa mawazo na ni kawaida yake kuvua nguo awapo kwenye hali hiyo
Taarifa zinasema, chumbani kwa kijana huyo kumekutwa kukiwa kumetapakaa damu nyingi pamoja na dawa za kutibu magonjwa ya zinaa na pombe kali.
EATV inafanya jitihada ya kuwasiliana na kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Lindi kujua kupata taarifa zaidi juu ya kisa hiki ambapo kwa sasa kijana Saimoni anapatiwa huduma katika wodi maalumu kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Sokoine huku Kaimu mganga mfawidhi Dkt Baraka Steven Mshango amekiri kumpokea kijana huyo akiwa na majeraha katika sehemu za siri huku sehemu ya uume wake ikiwa imetolewa kabisa