Jumamosi , 1st Jul , 2023

Mbunge wa jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya CCM Francis Mtega amefariki dunia leo mchana wakati akitoka shambani kwake kata ya Iyahi 

Inaelezwa kuwa Pikipiki aliyokuwa anaendesha imegangana na Power tiller lililokuwa limebeba shehena ya Mpunga kutoka shambani kuelekea kiiji cha Chimala. 

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amethibitisha ajali na kifo hicho ambapo ameandika 

"Kwa taarifa zilizonifikia hivi punde ... Mbunge Wa Jimbo La Mbarali Mh: Francis Leonard Mtega, Amefariki Dunia Mchana huu..kwa ajali ya pikipiki ikiwa na mhe mbunge ikigongana na pawatila
Hili ni Pigo CCM na serikali.
Pole kwa familia, pole kwa wanambarali, Pole kwa Ndugu jamaa na marafiki.
BWANA AMETOA, NA BWANA AMETWAA
JINA LAKE LIHIMIDIWE