Jumatano , 14th Jun , 2023

Isack Robertson (45) mkazi wa Sombetini jijini Arusha ambaye anakabiliwa na kosa la shambulio la kudhuru mwili ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya wilaya ya Arusha

Mshtakiwa huyo ambaye alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 31, 2023, mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Jenipher Edward anadaiwa kumpiga na kumjeruhi mkewe Jackline Mkonyi (38)

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mnamo Mei 23, 2023, majira ya saa tano usiku, eneo la Osunyai, Isack Robertson alimjeruhi mkewe, Jackline Mkonyi kwa kumng’oa jino kwa plaizi, kumpiga kwa mkanda usoni, mgongoni na maeneo mengine ya mwili 

Isack alitakiwa kuwa na Wadhamini wawili mmoja akitakiwa kuwa mtumishi wa serikali, wenye mali zisizohamishika, na sharti la tatu akiwatakiwa kutotoka nje ya mkoa wa Arusha baada ya kupatiwa dhamana.

Mshtakiwa Isack alitimiza masharti yote, ndipo hakimu Jenipher Edward akamuachi kwa dhamana na kuahirisha kesi hiyo hadi juni 29, 2023 na kuitaka jamhuri kuleta mashahidi siku hiyo