Jumanne , 1st Nov , 2022

Afisa msaidizi wa Kodi TRA, Chama Siriwa elimu ya mlango kwa mlango katika kampeni inayoendelea katika mkoa wa Simiyu kwa lengo kuelimisha wafanyabiashara wa mkoa huo sambamba na kuskiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu Bw. Gabriel Zakaria ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutumia Mbinu mbadala ya kuwadhibiti wafanyabiashara wadanganyifu, wanaowashawishi wanunuzi kutokudai risiti kwa madai ya kuwapunguzia bei ya bidhaa wanazonunua na kutoa risiti zenye thamani pungufu.

Ameyasema hayo alipotembelewa na ugeni wa Maafisa wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) uliongozwa na Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi, Bw. Julius Mjenga kwa lengo la kujitambulisha kwa Mkuu huyo kabla ya kuanza kwa zoezi la elimu ya mlango kwa mlango katika kampeni inayoendelea katika mkoa wa Simiyu kwa lengo kuelimisha wafanyabiashara wa mkoa huo sambamba na kuskiliza changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

Zakariya alianisha kuwa katika siku za karibuni kumekuwa na mbinu kadhaa zinazotumiwa na wafanyabiashara katika utoaji wa risiti halali jambo ambalo linasababisha upotevu wa mapato ya serekali.