Ijumaa , 23rd Sep , 2022

Umoja wa mataifa umesema kwamba vitendo vya ukatili wa kingono nchini Sudan Kusini vimekua vya  kawaida kiasi kwamba wanawake hawatoi tena taarifa za ukatili huo. 

Wanawake waliobakwa wamekosa huduma za dawa na ushauri ikiwemo wale waliobakwa na kundi la wanaume wengi kutokana na migogoro inayoendelea nchini humo. 

Umoja wa mataifa umeripoti kwamba baadhi ya wanawake wamebakwa mpaka mara tano katika kipindi cha miaka tisa iliyopita. 

Mwenyekiti wa jopo la umoja wa mataifa wanaojadili yanayojiri nchini Sudan kwenye kikao cha baraza la usalama la umoja wa mataifa jijini Newyork  Bi.Yasmin Sooka  amenukuliwa akisema kwamba “Hebu fikiria mwanamke mmoja anabakwa na kundi la wanaume wenye silaha, hebu fikiria kama ni wewe ama ni mtoto wako na tukio hilo linajirudia mara kwa mara’’   

 

Baadhi ya wanawake hubakwa wakati wakienda kutafuta kuni huku wakitishiwa kifo endapo watatoa taarifa za matendo hayo.