Jumatatu , 26th Jan , 2015

Mrisho Mpoto maarufu kama 'Mjomba' mwanamashairi maarufu nchini Tanzania ambaye pia ni mwanamuziki hii leo ameufungua mwaka kwa kutambulisha audio ya wimbo wake mpya alioubatiza jina 'Njoo Uichukue'.

Msanii wa mashairi na mwanamuziki nchini Tanzania Mrisho Mpoto

Mrisho amegusia moja ya mistari katika wimbo huu akisema 'Kwenye hela mkiweka picha zenu wekeni na za kwetu, kama hujui unapokwenda huwezi kupotea, wakati mnatumia mtutumie na sisi, huwezi kulala kwenye mto hata kama umekauka'

Aidha Mpoto ameitonya Enewz kuwa hivi sasa wapo katika mchakato wa kufanya shooting ya video wa wimbo huo kuanzia hapo kesho ambapo muongozaji maarufu Adam Juma ndiye atakayeisimamia kazi hiyo mpya.

Pata kionjo cha wimbo huo mpya 'Njoo Uichukue'.