Ijumaa , 23rd Jan , 2015

Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA imefuta usajili wa aina tano za dawa baada ya kubaini kuwa zina madhara na hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiit Sillo

Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA imefuta usajili wa dawa za binadamu aina Tano na kuamuru ziondolewe sokoni na vituo vyote vya kutolea huduma za afya mchini kote mara moja kutokana na kubainika kuwa na viambata vinavyosababisha maradhi sugu ikiwemo kiharusi, na wakati mwingine kusababisha vifo.

Dawa zinazotajwa kufutiwa usajiri na kuzuia uingizwaji kuwa ni pamoja na dawa za kutibu maralia ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine, dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na kapsulis zenye kiambata cha Fenil Propanolamine nyingine ni dawa ya sindano aina ya Chrolaphenical inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln cha nchini India, dawa za kutibu fungus ya vidonge na kapsuli.
 
Akitangaza dawa hizo mkurugenzi mkuu mamlaka ya chakula na dawa TFDA Bw. Hiit Sillo amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya uchunguzi wa kitaalam wa muda mrefu kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa ambao pia unafanya kazi kwa kutumia mtandao wa kimataifa kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO.
 
Aidha TFDA imefanya mabadiliko ya matumizi ya dawa ya maralia ya SP kutumika kama kinga ya maralia kwa wanawake wajawazito tu na kuagiza watengenezaji kubadili machapisho na vifungashio vyake mara moja ambapo mkurugenzi wa dawa TFDA Bw. Mitanga Fimbo pamoja na kufafanua athari anawataka watoa huduma nchini kote kuondoa dawa hizo na kuziteketeza mara moja kabla ya kuanza kwa msako.

Dawa aina Tano zilizofungiwa ni:-
Dawa ya kutibu Fungus ya vidonge na Kasuli aina ya Ketoconazole
Dawa ya kutibu Malaria ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine (Monotherapy)
Dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na Kapsuli zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanlo Amine
Dawa ya kuua bakteria ya sindano aina ya Chloramphenicol Sodium Succinate inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln Pharmaceuticals Ltd, India
Dawa ya Kuua bakteria ya maji na kapsuli aina ya Cloxacillin