Jumanne , 13th Jan , 2015

Jeshi  la  polisi  mkoa   wa  Mara  kwa  kushirikiana  na   wenzao   wa  nchi  jirani   ya  Kenya wamefanikiwa   kuwakamata  watu  wawili   kwa  tuhuma   za  wizi wa mtoto wa  miezi   saba.

Mtoto aliyekuwa ameibiwa akiwa na kamanda wa Polisi pamoja na mama wa mtoto

Jeshi  la  polisi  mkoa   wa  Mara  kwa  kushirikiana  na   wenzao   wa  nchi  jirani   ya  Kenya wamefanikiwa   kuwakamata  watu  wawili   kwa  tuhuma   za   kumwiba   mtoto   Diana Meshack   mwenye  umri   wa  miezi   saba   mkazi   wa  Makoko  katika   manispaa   ya  Musoma  kisha  kufichwa  nchini   humo   huku   waibaji   hao  wakiomba   kupewa  milioni tatu  ili  waweze   kumrejesha   mtoto  huyo.
 
Kamanda  wa  Polisi  wa  Mkoa  wa  Mara  ACP Philip  Alex  Kalangi, amesema  kuwa   mfanyakazi  wa  ndani   Paulina  Sobe   alikula  njama na kutoweka  na  mtoto  huyo  hadi  nchini   Kenya  kabla  baadhi   ya   watuhimiwa  hao  kuanza   kumpigia  simu  mama  mzazi    wa  mtoto  Gaudioza  Meshack   wakitaka  kutoa  kiasi  cha  shilingi  milioni  Tatu  ili  waweze  kumrejesha   mtoto  huyo.
 
Kamanda   Kalangi  amewataja   watuhumiwa  ambao  tayari   wamekamatwa   wakiwa  na  mtoto  huyo   huku  akisema  mfanya kazi  wa  ndani   bado  anatafutwa   na  kwamba taratibu   zimefanyika   za  kuleta   watuhumiwa  nchini  kwa  ajili   ya  hatua  zaidi  za kisheria ambao ni  Vicent Magesa  na Erick Range wote  wakazi  Getabwaga nchini Kenya.
 
Katika  siku   za  hivi  karibuni   kumekuwa  na  wimbi  kubwa  la  matukio  ya  wizi  wa watoto  ambao  umekuwa  ukifanywa  na  baadhi   ya  watu   wakiwemo  wafanyakazi  wa ndani  na  baada  kufanya   vitendo  hivyo   wamekuwa  wakilazimisha  kupewa  fedha kama  moja ya sharti  la  kurejesha  watoto  katika  familia  zao.