Jumatano , 3rd Dec , 2014

Rapa Kala Jeremiah ambaye historia yake katika chati za muziki haina rekodi yoyote ya yeye kuwasilisha ujumbe kuhusiana na maswala ya bata ama wakati mzuri, amesema kuwa hii inatokana na yeye kutokuwa mtu wa ratiba za kutoka na kufurahia maisha.

msanii wa miondoko ya bongofleva Kala Jeremiah

Kala ambaye kwa sasa amerejea katika chati na ngoma yake ya Usikate Tamaa akishirikiana na Nuruelly, amesema kuwa siku akijisukuma kufanya rekodi ya namna hiyo atakuwa anadanganya watu kutokana na kutokuwa na ufahamu wowote juu ya maisha haya ambayo vijana wengi wa mjini wanayapenda.