Jumatano , 26th Mei , 2021

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amesema kuwa alitamani mkoa huo uingie katika mikoa kumi bora nchini katika kuchangia pato la Taifa.

Brigedia Jenerali Marco Gaguti, Mkuu wa mkoa wa Mtwara

Akizungumza wakati wa kukabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu mpya wa mkoa huo Meja Jenerali Charles Mbuge, baada ya yeye kuteuliwa tena kuwa Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Gaguti, amesema Kagera bado ina fursa ya kufikia lengo hilo kutokana na kuwa na rasilimali nyingi na kupakana na nchi nne za Afrika Mashariki.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano pato la mkoa wa Kagera limepanda kwa asilimia 44 kutoka shilingi trilioni 3.7 hadi kufikia shilingi trilioni 5.3 za sasa, huku pato la mtu mmoja likipanda kwa asilimia 26.