Jumanne , 11th Mar , 2014

Staa wa muziki nchini', Chegge Chigunda, ameweka wazi kuwa katika historia ya muziki wake, anaiheshimu sana ngoma yake ya Twendzetu' ambayo ndiyo yenye mchango wa kumuweka katika chati akiwa anasimama peke yake pembeni ya kundi.

Chegge amesema kuwa, tangu alipotoa ngoma hii, aliweza kusimama mwenyewe hadi kutoa albam yake binafsi na kusimama kama mwanamuziki, ambapo staa huyu ametaka kuwakumbushia mashabiki wake kuwa katika historia ya muziki hawezi kusahau mchango wa ngoma hii classic 'Twendzetu'.