Akijibu swali la mbunge wa Tarime, Mh. Nyambari Chacha Nyangwine je ni lini wilaya za Tarime na Rorya zitatangazwa rasmi kuwa mkoa wa Mara Kaskazini kutokana na ukubwa wa jimbo la Tarime.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, Mhe. William Lukuvi amesema tume ya taifa ya uchaguzi inatarajia kutoa mwongozo kwa makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhusu vigezo na utaratibu wa kuzingatia katika kuwasilisha maombi ya kugawa jimbo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Amesema maombi yote ya kuanzisha mkoa mpya ni lazima yajadiliwe kwenye vikao vya kisheria vya mkoa na wakishakubaliana na hutakiwa kuwasilisha maombi husika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa baada ya uchambuzi wa waziri mkuu umshauri Rais ambaye ndiye mwenye dhamana na mamlaka husika.