
Zao la Alizeti
Wakizungumza na EATV wamiliki hao wa viwanda wameelezea athari za uhaba wa malighafi katika viwanda na jinsi watumiaji na wafanyabiashara wa mafuta wanavyoteseka kupata mafuta kwa wingi na kwa wakati.
Aidha wasimamizi hao wa viwanda, wameiomba serikali iwawezeshe wakulima ili waweze kulima kwa wingi alizeti, jambo ambalo litasaidia malighafi ipatikane kwa wingi na changamoto kama hizo zisiendelee kujitokeza.