Ijumaa , 7th Nov , 2014

Mrembo aliyewahi kuwa Miss Kenya, Shamim Nabil ameingia katika maisha mapya ya Mke na Mume, baada ya kufunga ndoa rasmi na aliyekuwa mchumba wake, Fahim Mohammed.

Miss Kenya Shamim Nabil akiwa na mumewe Fahim Mohammed

Mrembo huyu ameifanya harusi yake kuwa ni ya aina yake kwa kuisherekea kwa siku mbili mfulilizo, akianzia huko Zanzibar Tanzania kabla ya kwenda kumalizia uhondo nchini kwao Kenya.

eNewz inamtakia Shamim heri na furaha katika maisha yake haya mapya na mumewe huyu ambaye kazi yake ni Urubani.