Jumamosi , 1st Nov , 2014

Msanii wa Muziki anayefanya miondoko ya Soul na R&B kutoka Arusha, Hisia amezungumzia mapokezi mazuri ya aina ya muziki anaoufanya, kanda ya Kaskazini ambapo kuna misingi mizito ya muziki wa Hip Hop.

Hisia

Hisia ameweka wazi kuwa, Anajisikia vizuri kuona muziki wake ambao huwa anaupiga Live, unapokelewa na watu wengi siku hadi siku, na kuvutia hata wasanii wa Hip Hop ambao ndio wameshika soko la muziki Arusha.