
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobius Kifaru (Pichani).
Ofisa habari wa klabu hiyo, Thobias kifaru amesema kwa sasa timu yao haitoutumia tena Uwanja wa CCM Gairo, mara baada ya uongozi wa Klabu kwa kushirikiana na Chama cha soka kuufanyia ukarabati sehemu ya kuchezea na mahali pa kupumzikia wachezaji.
Pia amesema wanaamini mashabiki wao bado watendelea kwenda uwanjani kutazama mechi zao licha ya kwambo wameuacha uwanja wa CCM Shabiby uliopo Gairo.
Katika hatua nyingine Msemaji huyo amedokeza kuhusu mpango wa timu hiyo kujenga Uwanja wao wa kisasa ambao utakuwa karibu na makazi ya watu tofauti na hule wa Manungu ambao wenyewe upo mbali kidogo.
“Upo mpango mkakati mkubwa wa Klabu ya soka ya Mtibwa Sukari kujenga uwanja wa kisasa bora kabisa na hivi ninayozungumza nawe inawezekana juma hili shughuli ikawa imeanza ya kutengeneza uwanja bora wa kisasa ambao utakuwa wa aina yake katika viwanja bora vya Tanzania, “Thobius Kifaru.