
Zlatan Ibrahimovic amekutwa na Covid-19, hivyo ataukosa mchezo wa usiku wa leo wa Europa League dhidi ya Bodo Glimt
Zlatan mwenye umri wa miaka 38 amekutwa na maambukizi ya Covid-19 wakati wa vipimo vya raundi ya pili vya Covid-19 kwa wachezaji ambavyo vinapaswa kufanyika kabla ya mchezo ikiwa ni kanunu kwa wachezaji wote kupimwa kabala ya mchezo.
Klabu hiyo pia imethibitisha kuwa mchezaji huyo amejitenga mara moja, amewekwa karantini nyumbani lakini wachezaji wengine na wafanyakazi wa klabu hiyo hawajakutwa na maambukizi.
Ibrahimovic anakuwa mchezaji wa pili wa AC Milan kukutwa na maambuizi ya Covid-19 baada ya mlinzi wa klabu hiyi raia wa Brazil Leo Duarte kukutwa na maambukizi siku ya Jumanne katika vipimo vya raundi ya kwanza.
AC Milan itashuka dimbani Usiku wa leo katika uwanja wao wa nyumbani wa San Siro ambapo Milan watakuwa wenyeji wa Bodo Glimt ya Norway katika mchezo wa kufuzu wa michuano ya Europa League.