Alhamisi , 24th Sep , 2020

Mkurugenzi wa makampuni kutoka Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu, amewashauri vijana kuchangamkia fursa zilizopo vijijini badala ya kukimbilia mjini na kubaki kuuza manukato na nguo ambazo hazina wateja wengi.

Mkurugenzi wa makampuni kutoka Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 24, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio.

"Vijana wasiangalie fursa mjini, vijana wengi wakimaliza chuo wanafikiria kuuza perfume na nguo, vitu vinavyotumika na watu wa daraja la 3, nchi ina watu takribani Milioni 60 na wanaoweza kununua bidhaa hizo ni takribani Milioni 3", amesema Octavian Mshiu, Mkurugenzi wa makampuni kutoka TCCIA.

Aidha Octavian ameongeza kuwa, "Ningefurahi kuona wamachinga wanapungua na tuajiri zaidi kwenye maeneo yenye ujuzi, tuwe na watu wengi wenye ujuzi kuliko uchuuzi kwa sababu, tunapokuwa na watu wengi wachuuzi tunajenga uchumi wa nchi nyingine".