Alhamisi , 16th Jul , 2020

Kocha Jose Mourinho amethibitisha kumkosa mchezaji wake Tanguy Ndombele kwa mechi zote mbili zilizobaki kumaliza msimu.

Tanguy Ndombele akiwa katika kibarua chake kwenye moja ya mchezo wa ligi kuu ya England.

Ndombele aliumia goti walipokua mazoezini wakati Spurs ikijiandaa na michezo ya ligi inayoendelea hivi sasa.

Uthibitisho huo ulitolewa na Mourinho katika mahojiano yake na vyombo vya habari baada ya mchezo dhidi ya Newcastle ambapo  Tottenham iliibuka na ushindi wa 3-1.

Ndombele raia wa Ufaransa amecheza jumla ya dakika  64 tu , tangu kurejea kwa msimu  baada ya  kusimama kutokana na tatizo la Corona  pia inaelezwa hajawa na mahusiano mazuri na Kocha wake Jose Mourinho.

Awali kulikuwa na matumaini makubwa  toka kwa mchezaji huyu ghali aliyelipiwa paundi  milion  55 kama  ada ya uhamisho toka Olympic lyon lakini tangu ametua Spurs hajakidhi mahitaji ya timu.

Tottenham iliyoko kwenye nafasi 7 katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 55 wamebakiza mechi mbili tu  dhidi ya Leicester na Crystal Palace kumaliza msimu.