Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa Wavu nchini, Augustino Agapa amesema wameshatuma barua kwa vilabu mbalimbali shiriki vya michuano hiyo na wamevialika vilabu kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Agapa amesema michuano hiyo ilitarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu lakini kutokana na kuchelewa kuanza kwa michuano ya Wavu Klabu bingwa taifa iliyofanyika Septemba mwaka huu wameona wapeleke mbele michuano hiyo mpaka Novemba kwa ajili ya kuvipa nafasi vilabu shiriki kujiandaa kwa ajili ya michuano hiyo.