Alhamisi , 7th Mei , 2020

Mashabiki wa vilabu vikongwe hapa nchini Simba na Yanga, kutoka eneo la Kibirizi mkoani Kigoma ambao kwa miaka 10 mfululizo wamekuwa wakishindana katika kujitolea kuchangia damu salama, sasa wameanza kuhamasisha jamii.

Majengo ya makao makuu ya Simba na Yanga

Wameanza rasmi kwa pamoja mkakati wa hatua hiyo kwa kuihamasisha jamii ili ushabiki wa michezo uweze kusaidia kuokoa maisha ya watu.

Hamasa hiyo imeanza wakati Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania David David Mwakiposa, akiwa mkoani Kigoma wakati wa uzinduzi wa tawi la chama hicho, ambapo kwa pamoja wameahidi watapata mafunzo mengi ya kuisaidia jamii na kuweza kuwa na fursa ya uhamasishaji pia.

Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu akapongeza hatua hiyo na kusema ni mfano wa kuigwa na watu wengine ili utofauti wetu katika kushabikia mambo mbalimbali ikiwemo siasa na michezo yawe na manufaa kwa jamii.

Zaidi tazama video hapo chini