Jumanne , 28th Apr , 2020

Mtoto wa Binamu wa Jaji Mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhani, Yakud Ramadhani ameeleza kifo cha Jaji Ramadhani na kusema kuwa alikuwa anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, ambapo pia hata kabla ya mauti kumfika aliwahi kwenda kutibiwa nchini Kenya.

Marehemu Jaji Mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhani na mwanaye Yakud Ramadhan.

Hayo ameyabainisha leo Aprili 28, 2020, wakati akizungumza na Supa Breakfast ya East Afrika Radio.

"Ni kweli amefariki leo mida ya saa 2 asubuhi, alikuwa Aga khan na baadaye akaenda Kenya kwa matibabu zaidi na baadaye akarudi nyumbani lakini akawa bado anaumwa, sasa hivi wana familia wanafanya taratibu kwa chochote kitakachotokea tutawajuza" amesema Yakud.
 

Aidha kwa upande wa taarifa zilizotolewa na Mahakama ya Tanzania zimeeleza kuwa Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani, amefariki Dunia leo saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.