
Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa
Bashungwa aliyasema hayo mkoani Kilimanjaro alipofanya ziara katika kiwanda cha cha kuzalisha sukari cha TPC ili kujiridhisha na hali ya uzalishaji viwandani hapa.
Kuna viwanda vinne Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Kilombero Sugar na TPC wakati vinabinafsishwa vilipewa malengo ya kuongeza uzalishaji wake.
"Baada ya kutembelea TPC nawawatumia ujumbe viwanda vingine kama Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Kilombero Sugar kurejea mikataba ya ubinafsishaji ili kujiridhisha kama wanaenda sambamba na mikataba hiyo."
"Kama watakuwa wameshindwa kutimiza malengo hayo basi watakuwa wanatukwamisha, Rais Dk John Pombe Magufuli alipoingia madarakani mwaka 2015, aliweka malengo ya kuwa nchi ya viwanda ili tujitegemee katika uzalishaji wa vitu kama sukari."