Ijumaa , 20th Dec , 2019

Leo Disemba 20, 2019 ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa msanii na mfanyabiashara Shilole, ambaye amesema unavyofurahia siku yako ya kuzaliwa, basi hata siku zako za kuishi duniani zinakaribia kuisha.

Msanii wa Muziki na Filamu, Shilole.

Akiieleza EATV & EA Radio Digital, Shilole amesema haoni haja ya kufanya party kubwa kama walivyo mastaa wengine, ambao ikifika siku zao za kuzaliwa, kwao wanafanya kama sherehe.

"Kama umeona birthday yangu ya mwaka jana sijafanya chochote zaidi ya kwenda kutoa vitu kwa watu wenye uhitaji kwahiyo sihitaji sherehe, mtu bado una miaka 30 na kuendelea halafu unataka kufanya sherehe tuachane tu na hayo mambo, halafu siwezi kuwekeza pesa yangu kwenye birthday bora nifanye vitu vingine vya maendeleo" amesema Shilole.

Aidha Shilole ameendelea kusema "Unapofurahi birthday yako ujue hata siku yako ya kufa inakaribia, masuala ya kufanya sherehe sioni kama kuna sababu au labda mimi najiona nimekuwa siwezi kufanya party unaweza ukafanya vitu vidogo nyumbani kwako na watoto wako shughuli ikaisha" ameongeza.

Hii hapa ni orodha ya mastaa wa kike, waliozaliwa Disemba akiwemo, Shilole, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na Esha Buheti.