Dkt Benson Bana
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, dakika kadhaa mara baada ya kutangazwa kuteuliwa kwake, Dkt Bana amesema taarifa hizo amezipata akiwa ndani ya gari lake na amepanga kwenda Kanisani kumshukuru Mungu.
''Sikutarajia kwahiyo ni furaha kubwa, kila kitu kinachotokea Mungu anakusudio lake, nimezipata nikiwa barabarani nikiwa naendesha gari yaani hadi sasa hivi kuna watu kama 30 wamenipigia simu, natafakari maisha baada ya tukio hilo, ngoja nitafakari niende kanisani nikasali kidogo na nikashukuru Mungu basi'', amesema Dkt Bana.
Uteuzi huo wa Dkt Bana umetangazwa leo Septemba 20, 2019 na Katibu mkuu kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi.

