Ijumaa , 20th Sep , 2019

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, amesema bado Serikali inadaiwa na Wakulima wa Korosho Shilingi Bilioni 50, kufuatia kununua Korosho katika msimu uliopita, kufuatia kuibuka kwa sintofahamu ya uuzaji.

Waziri Hasunga, ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, wakati akitangaza juu ya ujio mpya wa uuzaji wa zao la Korosho, ambapo wanunuzi wa zao hilo watalazimika kujisajili kwa njia ya mtandao na kueleza mahitaji wanayoyataka.

"Kuna Korosho ambazo tulibangua ndani na nyingine tunaendelea kubangua ndani, lakini kwa thamani ya Korosho zote kwa msimu uliopita tulitakiwa kulipa Bilioni 723, lakini mpaka sasa tunadaiwa Bilioni 50, na shghuli ya kuwalipa bado inaendelea na tutahakikisha tunawalipa." amesema Hasunga

Kuhusiana na mfumo mpya uuzaji wa Korosho Waziri Hasunga amesema kuwa "baada ya uzoefu wa mwaka jana kwanza tutaendesha minada ya wazi, lakini sasa itakuwa ya wazi na kila mwananchi anaona, na minada hii itaonwa Duniani kote, na msimu tutazidua rasmi Septemba 30, 2019, mtu yeyote au Kampuni inayotaka kununua korosho kujisajili kwenye mfumo kompyuta ya Wizaraya Kilimo."

Tazama video hapo chini